Ijumaa 29 Mei 2026 - 16:00
Waustralia Wameingia Barabarani Kuiunga Mkono Meli ya Sumud

Hawza/ Wanaharakati wa masuala ya kibinadamu siku ya Jumanne walifanya mkusanyiko wa maandamano katika jengo la Bunge la Australia kupinga namna ambayo utawala bandia wa Israel ulivyowatendea wanachama wa Msafara wa Kimataifa wa Sumud, juhudi za watu hao zilikuwa ni kufikisha misaada ya kibinadamu kwa wananchi wa Ghaza pekee, watu waliohudhuria katika bunge hilo waliitaka serikali ya Australia kuiwekea vikwazo utawala huo wa umwagaji damu wa Israel.

Kwa mujibu wa kitengo cha tarjuma cha Shirika la Habari la Hawza, waandamanaji walikusanyika katika ukumbi wa marumaru wa bunge hilo na wakapiga magoti huku mikono yao ikiwa nyuma ya migongo yao ili kuonesha namna wanaharakati wa Msafara wa Sumud walivyowekwa kizuizini na mamlaka ya utawala dhalimu wa Kizayuni.

Walikuwa wakipaza sauti wakisema: “Iwekeeni Israel vikwazo!” na wakamtuhumu Waziri Mkuu Anthony Albanese pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje Penny Wong kuwa washirika katika jinai za utawala wa Kizayuni dhidi ya ubinadamu, huku maafisa wa usalama wakiwalazimisha kutoka nje ya jengo la bunge na wanaharakati hao wakiendelea kupaza kaulimbiu zao.

Maandamano haya yalifanyika baada ya kuongezeka kwa mjadala kuhusu mienendo isiyo ya kibinadamu dhidi ya wanaharakati wa haki za binadamu na tukio lililotokea katika msafara wa baharini wa Sumud.

Suala hili lilipata umakini mkubwa zaidi baada ya Itamar Ben-Gvir, Waziri wa Usalama wa Taifa wa utawala bandia wa Israel, wiki iliyopita kusambaza video katika mitandao ya kijamii ambayo ndani yake aliwadhihaki wanaharakati waliokamatwa wa Msafara wa Sumud, maafisa wa Australia waliwasukuma baadhi ya waandamanaji na kuwaburuza chini, jambo ambalo liliporipotiwa t
na vyombo vya habari lilisababisha kulaaniwa duniani kote.

Chanzo: Shirika la Habari la Anadolu

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha